1. Forum
  2. >
  3. Topic: Swahili
  4. >
  5. Swahili Practice for Novices

https://www.duolingo.com/profile/Joana_AA

Swahili Practice for Novices

Jambo! Jina langu ni Joana. Nina umri wa miaka kumi na nane na ninatoka Accra, Ghana. Na wewe?

September 8, 2017

16 Comments

Sorted by top post

https://www.duolingo.com/profile/Joana_AA

Ninaona ninaona. Ni saa sita za mchana hapa, lakini nisipoweza kulala, ninatazama televisheni: Suits au Game of Thrones. Unaangalia ama? PS: 'nisipoweza' - nilitumia nzuri?

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Sitazami Game of Thrones. Ninajua kwamba nikianza kuitazama, sitaweza kuacha. Nilimaliza kutazama Orange is the New Black karibuni, na sasa hivi sitazami televisheni au Netflix na kadhalika - ninafanya muziki, kusoma au kuandika, au kutazama video kwenye YouTube ...

Na ndiyo - ninadhani kwamba ulitumia "nisipoweza" vizuri. :-)

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/Joana_AA

Halafu, ninapenda picha yako! Uliichora?

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Asante sana! Hapana, sikuichora. Niliiona kwenye Internet nikaiiba. ;-) Inaonekana kama mimi kidogo, lakini labda uso wangu si mzuri sana kama picha haha.

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/Joana_AA

Hakunamatata. Unafanya kazi Ujerumani?

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Ndiyo. Mimi ni msaidizi wa mawasiliano. Bosi wangu ni kiziwi na mimi hutafsiri kidogo na vilevile huandika makala kwa ajili ya tovuti.

September 10, 2017

https://www.duolingo.com/profile/Joana_AA

Hiyo inaonekana kuvutia. Natumaini hutumia faida yake :-] Pia, una mke au watoto?

September 10, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Sina mke, sina mume, sina watoto, sina mpenzi ... niko peke yangu, lakini nina rafiki wengi wazuri. :-) Na wewe je?

September 10, 2017

https://www.duolingo.com/profile/rokksolidrees

VP Hali, natoka Marekani, katika Jimbo la Ohio. Sasa ni usiku, saa sita kasoro robo. Nilitazama Game of Thrones kidogo, lakini sipendi. Mimi hupenda kutazama Dragon Ball, sasa hasa Dragon Ball Super. Nina miaka Ishirini na nne.

September 11, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Sijambo, Joana! Ninaitwa Ben. Nina miaka thelathini na mitatu. Ninatoka Australia, lakini sasa nimeishi Ujerumani kwa miaka minne. Ni usiku hapa, lakini siwezi kulala. Unafanya nini usipoweza kulala?

September 9, 2017

https://www.duolingo.com/profile/rokksolidrees

Unaposema idadi zaidi ya tano, usiseme "mi-" kabla ya tatu. Hata hivyo tatu chini ya tano, thelathini na tatu zaidi ya tano. Kwa hiyo, Sema "thelathini na tatu." Sawa? Tunasaidiana!!

September 11, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Namba ni hivyo:

-moja
-wili (mbili)
-tatu
-nne
-tano
sita
saba
-nane
tisa
kumi

(Kistari kionyesha kwamba viambishi awali vinatumiwa.)

Namba kubwa zaidi ni hivyo:

kumi na -moja
kumi na -wili (kumi na mbili)
kumi na -tatu
kumi na -nne
kumi na -tano
kumi na sita
saba
kumi na -nane
kumi na tisa
ishirini
ishirini na -moja
ishirini na -wili (ishirini na mbili)
ishirini na -tatu
ishirini na -nne
ishirini na -tano
ishirini na sita
ishirini na saba
ishirini na -nane
ishirini na tisa
thelathini
thelathini na -moja ... na kadhalika

Mifano:

...
watu ishirini na wanane (watu 28)
watu ishirini na tisa (watu 29)
watu thelathini (watu 30)
watu thelathini na mmoja
watu thelathini na wawili
watu thelathini na watatu
watu thelathini na wanne
watu thelathini na watano
watu thelathini na sita
watu thelathini na saba
watu thelathini na wanane
watu thelathini na tisa
watu arobaini
watu arobaini na mmoja
watu arobaini na wawili
...
watu elfu moja mia mbili ya mmoja (watu 1,201)
watu elfu moja mia mbili ya wawili (watu 1,202)
...
viazi ishirini na tisa (viazi 29)
viazi thelathini
viazi thelathini na kimoja
viazi thelathini na viwili
viazi thelathini na vitatu
...

September 11, 2017

https://www.duolingo.com/profile/rokksolidrees

eeeeh, labda hivi kewli. Lakini, najua watu ambao wanasema "nina miaka ishirini na nne" "mayai kumi na mbili." Maybe, because proper Swahili is rarely spoken by Swahili speakers, this is true, but not commonly practiced.

September 12, 2017

https://www.duolingo.com/profile/AGreatUserName

Watu waliowengi wanaozungumza Kiswahili si wazungumzaji asilia.

September 12, 2017

https://www.duolingo.com/profile/Fateem13

Ni kweli kabisa kwamba watu wengi hawaongei kiswahili hasa. Mimi ni mmoja wao, mimi ni mtanzania lakini Swahili ni bovu. Ni slang na a mix of two other languages (kutchi and English). Sadly, this is common in a lot of the younger generation ndio maana niko hapa kujifunza kiswahili hasa halafu nitamfundisha mtoto wangu.

Nimefurahi kusoma Swahili lenu

September 25, 2017

https://www.duolingo.com/profile/rokksolidrees

Aha, unasema "viazi ishirini na vinne" kweli, lakini watu wengi wanasema "viazi ishirini na nne." Or wanasema "viazi nne?" Nilipojifunza, walisema "viazi nne" ni Kiswahili kibaya, nahitaji kusema "vinne." Lakini sikuzote nilisikia "ishirini na nne" bila vi-.

September 25, 2017
Learn Swahili in just 5 minutes a day. For free.